Jumamosi, 7 Aprili 2018

MWENYE KUOMBA DUA NYAKATI HIZI ATAKUBALIWA TU.


ADABU ZA KUOMBA DUA.



Sifa njema zinamstahikia Allah Mola wa ulimwengu. Rehma na amani zimshukie mtume wa Allah (s.a.w). Ama baada ya utangulizi huu mfupi, huu ni mwendelezo wa darsa za dua sehemu ya pili. hapa utajifunza kuhusu adabu za kuomba dua. itambulike kuwa dus yenye sifa za kukubali wa na Allah ni lazima zifate taratibu zilizowekwa na adabu zake. unaweza kupata darsa zote za dua kupitia simu yako ya kiganja. ingia play store kisha andika darsa za dua. au >>bofya hapa>> kudowanload App usome dua mbalimbali.
Tumeona katika darsa zilizopita kuhusu adabu za kuomba dua bofya hapa kusoma pamoja na fadhi la za dua bofya hapa kusoma na mengine. leo tutaona nyakati ambazo ni mahususi kuomba dua.

                      NYAKATI AMBAZO DUA HUJUBIWA.
1.Theluthi ya mwisho ya usiku. Huu ni usiku wa manane usiku mkubwa. Muda huu mweye kuomba dua katu haiwezi kurudi kama anavyosimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema  "‏ يَنْزِلُ رَبُّنَا كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الآخِرُ فَيَقُولُ مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ وَمَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ وَمَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ ‏"
“anashuka Mola wetu aliye tukuka kuja mbingu ya dunia kila usiku pindi inapobaki theluthi ya usiku ya mwisho kisha husema ‘nani ataniomba nimjibu maombi yake, nani antaniomba nimpe na nani ataniomba msamaha nimsamehe”. (amepokea Bukahari, muslim na wengine).

2.Baada ya swala za faradhi. Anayetaka kuomba dua basi aombe baada ya kuswali swala ya faradhi, dua yake itajibiwa. عَنْ أَبِي أُمَامَةَ، قَالَ قِيلَ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَىُّ الدُّعَاءِ أَسْمَعُ قَالَ ‏"‏ جَوْفُ اللَّيْلِ الآخِرُ وَدُبُرَ الصَّلَوَاتِ الْمَكْتُوبَاتِ ‏"‏ 
Amesimulia Abuu Umama  رضىالله عنه kuwa aliulizwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم ‘dua gani husikulizwa (zaidi na Allah? Akasema:) usiku mkubwa (theluthi ya mwisho ya usiku) na baada ya swala za faradhi’”. (amepokea tirmith kwa isnad sahihi).



3.Kati ya adhana na iqama. Huu ni muda unaopatikana baada ya kuadhiniwa na mpaka kukimiwa kwa swala. Hapa mwenye kuomba dua itakuwa ni yenye kujibiwa. Amesimulia Anas رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “hairudishi (haiachi kujibiwa dua) kati ya adhana na iqama”. (amepokea Abuu Daud, Nisai na tirmith kwa isnad sahihi).

4.Wakati wa kusujudi. Hii ni dua inayoomwa wakati mtu akiwa amesujudi, dua hii pia ni yenye kujibiwa. Amesimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “muda ambao mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake ni pale akiwa amesujudi. Basi zidisheni dua (muda huu) na uweni na uhakika kuwa mtajibiwa. (amepokea Muslim na Daud).

5.Muda wa kukutana majeshi kwenye jihad, muda wa kunyesha kwa mvua, muda wa kukimiwa kwa swala na na muda wa kuiona alkaba. Amepokea Abuu Umamah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema: “hufunguliwa milango ya mbinguni na hujibiwa dua katika maeneo manne (nyakati): muda wa kukutana safu katika jihadi, muda wa kunyesha kwa mvua, muda wa kukimiwa kwa swala na muda wa kuiona alkaba”. (amepokea Tabrany).



6.Siku ya ijumaa. Siku ya ijumaa kuna muda ambao dua hujibiwa bila ya tatizo. Muda huu ni mchache sana na hakuna anaoujua. Zipo riwaya nyingi sana zinataja muda huu. Ila kuna riwaya zinaonesha muda huu ni baada ya swala ya al-’asr mpaka magharib. Ila ukweli ni kuwa muda huu ni mchache sana na haujulikani, jambo la msingi ni kujitahidi kumuomba Allah siku ya ijumaa yote huenda muda huo ukaupata.

Unaweza kusoma darsa zote za dua katika simu yako ya kignja bofya hapa. In Shaa Allah panapo majaaliwa tutawaletea darsa za qurani pamoja na tajweed. tunanamuomba Allah atupe wepesi juu ya hili. pia tunathamini mchango wenu ndugu wasomaji pindi utakapoona kosa lolote katika darsa zetu tunaomba utuelekeze ama kama una jambo unataka kuchangia tafadhali wasiliana nasi kwa namba +255 675 255 927 kama hautatupata tutumie sma kwa nmba hiyohiyo au barua pepe rajabumahe@gmail.com.


UHIMU KWA AJILI YAKO
Jifunze zaidi kuhusu Afya yako na lishe ukiwa na program zetu kwenye simu yako ya kiganja. bofya link zifua tazo kupata elimu zaidi juu ya afya yako
1.Afya na lishe bofya hapa
2.afya yako. bofya hapa
3.kupata post zetu moja kwa moja . bofya hapa



NYINGINEZO